10 Julai 2026 - 23:38
Mamia ya Watunisia Waandaa Mazishi ya Mfano kwa Heshima ya Kiongozi Shahidi Imam Sayyid Ali Husseini Khamenei

Mamia ya wananchi wa Tunisia walifanya mazishi ya mfano kwa heshima ya Kiongozi Shahidi Imam Sayyid Ali Husseini Khamenei, wakithibitisha mshikamano wao na mhimili wa muqawama na kupinga kuhalalishwa kwa uhusiano na utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Mamia ya wananchi wa Tunisia wamefanya mazishi ya mfano au ishara kwa heshima ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Shahidi Sayyid Ali Husseini Khamenei (Mwenyezi Mungu aitakase roho yake).

Hafla hiyo ilifanyika kufuatia mwito wa vyama na mikondo mbalimbali ya kisiasa na kijamii inayopinga kuhalalishwa kwa uhusiano na utawala wa Kizayuni. Washiriki walikusanyika kwa wingi wakionesha huzuni yao na kutoa heshima kwa kiongozi huyo, huku wakisisitiza kuendelea kuunga mkono mhimili wa Muqawama na mapambano dhidi ya dhuluma.

Katika mazishi hayo ya ishara, washiriki waliinua bendera nyeusi pamoja na mabango yaliyokuwa na kaulimbiu "Simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu" na "Ewe waliolipiza kisasi cha Imam Husayn (a.s.)", wakieleza kuwa wataendelea kushikamana na maadili ya Uislamu, haki, uadilifu na kupinga ubeberu pamoja na utawala wa Kizayuni.

Washiriki pia walisisitiza kuwa kumbukumbu ya viongozi na mashahidi wa muqawama itaendelea kuishi katika nyoyo za Waislamu na watu wote wanaopigania uhuru na haki duniani. Mazishi hayo ya mfano yalikuwa ishara ya mshikamano wa wananchi wa Tunisia na mataifa yanayopinga ukandamizaji na kuunga mkono kadhia ya Palestina.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha